
NA JOSEPH MSAMI, NEW YORK
Simba msipotulia , mtalikoroga
Ni
kawaida kwa timu za Simba na Yanga na kwa ujumla timu nyingi kuchukua
hatua pale mambo yanapoenda mrama mathalani vipigo mfululizo, kukosa
kombe kwa muda mrefu, kufungwa na timu yenye uwezo mdogo na kwa ujumla
matokeo mabaya na yasiyotarajiwa.
Kwa
bahati mbaya sana Simba na Yanga za Tanzania zinakabiliwa na shinikizo
kubwa la mashabiki na wanachama jambo linaloweza kuzifanya kuamua mara
nyingine hata kumfukuza kocha kwa vile tu kelele zimezidi. Uamuzi kama huo waweza kuwa namatokeo chanya u hasi kwa timu husika.
Juma hili limekuwa baya kwa Simba kufuatia kufungashwa virago kwenye kombe la Mapinduzi baada ya URA ya Uganda kuifunga kwa bao 1-0. Awali Simba ilipokea kipigo cha bao hilohilo moja kutoka kwa Azam ya Tanzania.
Vipigo
hivyo vimeleta tafrani na kwa yeyeote anayefahamu soka la Bongo,si
ajabu ukasikia Simba wanasaka mchawi, yaani kuwachnguza nani
wametufungisha na hata kuanza kujadili uwezo wa kocha na ikibidi
kumfukuza.
Wachezaji waweza kuathirika
Katika
hatua kama hizi, mara kahdaa wachezaji wamekuwa watuhimiwa namba moja.
Huonekana wasaliti au wahujumu kwa namna moja au nyingine .Sisemi kwamba
hakuna wachezaji wanaohujumu timu.
Lakini
swali la kujiuliza ni kwamba hivi kwanini timu hizi au soka letu kila
unapofanya vibaya kuna mchawi? Siku moja nikiwa nimesononeka sana baada
ya timu ninayoishabikia huko Ulaya kufungwa, nilimpigia simu rafiki
yangu akaniambai maneno ambayo hata leo nayakumbuka. Alisema, “No King
rules forever” Akimaanisha hakuna mfalme anayetawala au kudumu milele.
Huwa
najiuliza hivi vilabu vikubwa duniani kama vile Real Madrid ambayo hivi
karibuni ikicheza na hasimu wake mkubwa Barcelona ilichapwa kipigo cha
aibu ikiwa nyumbani cha 3-1, wao hawapigiwi kelele tulizozoea kuzisikia
kwetu? Mbona hawafanyi haraka kufukuza na kusaka wachawi?
Ikiwa
timu hizo zisingejenga utamaduni wa uelewa kuwa mpira hudunda na kwamba
kuna matokeo ya suluhu, sare, kufungwa na kufunga, nadhani kungekuwa na
mtiti ndani ya timu na labda mchezaji ambaye ni tumaini
kama Christian Ronaldo ambaye siku ile hakufanya alichotarajiwa,
angeonekana kafanya figisu.
Wakati fulani wachezaji kama vile beki wa Yanga Kelvin Yondani, (aliyewahi
kuchezea Simba) na hata kiungo Nurdin Bakari aliyekuwa Simba kabla
waliwahi kutuhumiwa kuzihujumu timu kwa kile kilichoitwa wana mapenzi na
timu pinzani.
Miongoni
mwa waathirika wakubwa ni Henry Joseph wa Mtibwa, mchezaji aliyewahi
kuwa tegemeo la timu ya Taifa na kapteni wa timu hiyo. Wakati akiwa
Simba alilazimika kucheza kufa na kupona kuzishinda sauti na kejeli za
mahaba yake na Yanga. Kila ilipofika wakati wa mchezo kati ya watani wa
jadi Henry alijikuta ana wakati mgumu kwani kosa la kawaida lilimgharimu vilivyo.
Nimeeleza
kwa urefu hayo kwakuwa nataka kusisitiza kuwa yawezekana kabisa kuna
wachezaji wasaliti, lakini ikiwa hisia zitatokana na shinikizo la
mashabiki, matokeo yake huharibu timu na kupoteza mwelekeo.
Simba yaweza kuboronga isipomakinika.
Baada
ya kutolewa kwenye kombe la Mapinduzi, ikiwa benchi la ufundi la
wekundu wa msimbazi halitatambua wajibu wa tathimini ya kitaalamu na
kuchukua hatua kurekebisha mapungufu, na kuruhusu fitna, wataenda nazo
ligi kuu, na huo huenda ukawa mwanzo wa timu kufanya vibaya na kulikosa
kombe ambalo kwao kwa sasa ni A must win season.
Yaani ni msimu ambao kwa namna walivyowekeza kununua wachezaji na kuanza kwa kasi, wameshajiongezea deni la kubeba ubingwa .
Mitandao ya kijamii, wanachama na mashabiki.
Naelewa
vyema kwamba timu hizi yaani Simba na Yanga na nyinginzeo zina
wanachama kwa mujibu wa katiba na sheria. Sitaeleza leo kwa kirefu,
faida na hasara ya kuwa na wanachama, sina maana ni jambo baya la msingi
ni nguvu waliyo nayo na mipaka yao.
Ninachotaka
kusema hapa ni kwamba pamoja na wanachama na mashabiki kupiga kelele
nyingi kupitia mitandao ya kijamii na njia nyinginezo, benchi la ufundi
na uongozi wa Simba una wajibu wa kujali mustakabali wa timu kwa
kuzingatia na kusoma alama za nyakati.
Kweli,
wanachama hawapaswi kupuuzwa kwa kuwa ni wanahisa, wakati huo huo
ukiamua kwa shinikizo waweza kufanya uamuzi mbaya. Kwa mfano maoni
kwamba chanzo cha kuboronga kwa Simba ni kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha
Joseph Omog yaweza kuwa sahihi au siyo sahihi, lakini kuamua kumrudisha
yaweza kuleta mgawanyiko mkubwa na kuongeza sintofahamu zaidi ndani ya
klabu.
Kocha Irambona Masoud Djuma
Nimesoma
lawama za mashabiki na pengine wanachama kwa kocha msaidizi Irambona
Masoud Djuma ambaye ndiye kashikilia benchi la ufundi kwa sasa, kwamba
mfumo wake haueleweki na si imara katika ulinzi na pengine wakashinikiza
kuwa afukuzwe.
Hili
ni kosa ambalo ikiwa Simba watajaribu kulifanya nabashiri watapotea na
kama usemvayo usemi wa Kiswahili vita vya panzi furaha ya kunguru,
mahasimu wao Yanga watajinufaisha na mgogoro huo na kuwaondoa kwenye
muelekeo wa ushindi na pengine hata kushinda. Timu nyingi hasa za nchi
zilizoendelea kisoka hufanya uamuzi huo pale inapobidi na hakuna namna
nyingine, kwani huelewa madhara yake katika mfumo wa uchezaji na
wachezaji wenyewe.
Kwa
maoni yangu kufungwa mara mbili mfululizo yaani dhidi ya Azam na URA
kwenye kombe la Mapinduzi kuwe chachu kwa Simba kuimarisha uwezo wake
kuelekea ligi kuu ambayo inaongoza, badala ya kutumia muda mwingi kusaka
mchawi eti kwa kuwa Yanga wamefanya vyema badi kuna mkono wa mtu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni