Jumapili, 7 Januari 2018

JOTO LAZUA BALAA AUSTRALIA



Mji wa Sydney nchini Australia umekumbwa na hali ya kiwango cha juu cha joto ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa kipindi cha miaka 79 iliyopita kwa kufikia nyuzi joto 47.3
Eneo la Penrith magharibi mwa Sydney wenyeji walitafuta hifadhi katika baada ya maeneo ya mji huo uliokubwa na kiwango hicho cha juu cha joto leo Jumapili.
Viwango vya joto vimekaribia vile vilivyowahi kutokea mwaka 1938 vilivyofikia nyuzi joto 47.8.
Katika mashindano ya Kimataifa ya Tennis yanayoendelea katika mji wa Sydney nayo yamelazimika kusimama kutokana na joto kali hilo lililozidi nyuzi joto 40.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni