Jumapili, 21 Januari 2018

Dili la wa Mkhitaryan, Sanchez lakaribia kukamilika



 aada ya michezo yao ya  jana kauli za makocha wa timu za Arsenal, Arsene Wenger na Manchester United, Jose Mourinho zilionesha kuwa usajili wa wachezaji Alexis Sanchez na Henrikhi Mkhitaryan uko mbioni kukamilika.

"Sanchez hakucheza kwa sababu huwezi kusafiri kwenda Kaskazini na kucheza mpira wa miguu wakati huo huo," alisema Wenger wakati akijibu swali alipoulizwa kwanini Sanchez hakucheza kwenye ushindi wa 4-1 iliopata Arsenal dhidi ya Crystal Palace.

Kocha wa Man United Jose Mourinho yeye alipoulizwa kuhusu usajili wa Sanchez, alijibu kwa kifupi ''upo karibu kukamilika''. Jibu hilo la Mourinho lilionesha wazi kuwa makubaliano kati ya pande hizo mbili yamekamilka ambapo Henrikh Mkhitaryan wa United atakwenda Arsenal.

Katika msimu mmoja na nusu ambao Mkhitryan ameichezea Man United amefanikiwa kufunga mabao matano na kusaidia mengine sita huku Sanchez akifunga mabao 60 na kusaidia mengine 25 katika misimu mitatu na nusu aliyoicheza Arsenal.

Ripoti mbalimbali kutoka nchini England leo zinaripoti kuwa huenda nyota hao wawili Mkhitaryan raia wa Armenia na Sanchez raia wa Chile watafanyiwa vipimo ili kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu zao mpya.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni