Mfungwa
mmoja amezinduka na kujikuta yupo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
baada ya madaktari watatu kuthibitisha kuwa alikuwa amefariki, vyombo
vya habari Uhispania vimetoa taarifa hiyo.
Gonzalo Montoya Jiménez alikuwa ni
mfungwa katika gereza Asturias na alizinduka saa chache kabla ya
kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kugundua chanzo cha kifo chake.Gonzalo yupoa chini ya uangalizi wa madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Oviedo. Mmoja wa ndugu zake ameliambia gazeti la La Voz de Asturias kwamba Gonzalo “alikuwa amewekewa alama ya kufanyiwa upasuaji, tayari kupasuliwa”.
Wataalamu wamesema hali hiyo inaitwa ‘catalepsy’ ni hali ambayo ishara muhimu za uhai hufifia kwenye mwili wa binadamu kiasi cha kutoweza kutambulika kama yupo hai.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni