Jumatano, 24 Januari 2018

AZAM, YANGA KUPIGWA SAA 10 CHAMAZI



Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam FC na Young Africans uliopangwa kuchezwa saa 1 usiku sasa utachezwa saa 10 jioni kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo huo ambao Azam Fc ndio wenyeji wa mchezo huo kwa ratiba ya Bodi ya Ligi ilitakiwa kuchezwa saa 1 usiku ,kutokana na Ukubwa wa Mechi hiyo na Usalama zaidi mda umesogezwa nyuma na mchezo huo utachezwa saa 10.00 jioni.
Viingilio kwenye mchezo huo ni shilingi elfu kumi(10,000) kwa Jukwaa Kuu na shilingi elfu saba (7,000) kwa majukwaa ya kawaida.
Pia Waamuzi wa mchezo huo wote ni kutoka Jijini Dar es Salaam ambapo muamuzi wa kati ni Israel Nkongo akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na mwamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila, mwamuzi wa akiba Elly Sasii wakati Kamishna wa mchezo huo ni Omar Abdulkadir

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni