
Kapteni wa timu ya Azam FC, Himid Mao amesema kwamba wanategemea ushindi
katika fainali za Kombe la Mapinduzi linalotarajiwa kufanyika Jumamosi
ya Januari 13.
Akizungumza kutokea Zanzibar, Mao amesema kwamba wanaamini kuwa timu watakayocheza nayo, URA ni timu ambayo ipo vizuri hivyo hivyo ni lazima wajitahidi kwa kadri wawezavyo ili kuleta ushindi.
Aidha kwa upande wake Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioba amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya fainali dhidi ya URA ya Uganda na wanaamini maandalizi ndiyo yaliyowafikisha hapo
"Tumefika hapa kutokana na maandalizi na timu nzima kujituma, tunajua mechi ya fainali itakuwa ngumu zaidi kwa kuwa URA watakuwa na mbinu tofauti. Sisi tuko tayari na tutaendelea kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi hiyo," amesema Cioba
Azam FC ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano hiyo baada ya timu zote za Tanzania Bara na Visiwani, kung'olewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni