Jumapili, 21 Januari 2018

ACT Wazalendo wametangaza kujitoa kwenye Marudio ya Uchaguzi



 Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu wake Bara Msafiri Mtemelwa kimetangaza kutoshiriki Uchaguzi mdogo wa marudio katika Majimbo ya Kinondoni na Siha.


 January 21, 2018 Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa Ubunge Kinondoni na Siha na Kata za Udiwani February 17, 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwepo uwanja mpana wa mapambano.
Akiongea na Waandishi wa Habari Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo bara Msafiri Mtemelwa amesema moja ya sababu ya kutoshiriki ni kutokana kuwepo kwa mapungufu katika chaguzi ndogo zilizopita ikiwemo baadhi ya viongozi wa umma kuingilia uchaguzi, jeshi la polisi na Wakurugenzi.
“Sisi ACT Wazalendo tunaendelea na kutoshiriki kwa sababu bado hatujapata uhakika wa uwanja wa mapambano, Tume ilikutana na wadau na walikiri na kusema wameanza kukemea Wakuu wa Wilaya na Mikoa wasishiriki,” -Mtemelwa

 Mtemelwa alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mazingira ya Uchaguzi ambayo waliyalalamikia kwa Tume ya Uchaguzi hayajafanyiwa marekebisho.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni