Timu
ya taifa ya Zanzibar imeibuka bingwa wa kwanza wa michuano ya soka la
ufukweni inayofahamika kwa jina la Copa Dar es salaam.
Michuano hiyo iliyofanyika kwa siku mbili katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam imemalizika leo kwa kushuhudia Zanzibar ikiichapa Malawi mabao 3-2 katika mchezo wa fainali.
Wakati Zanzibar wakiwa mabingwa, ndugu zao Tanzania Bara imeambulia nafasi ya tatu baada ya kuichapa Uganda mabao 5-4 katika mchezo uliotangulia, na hivyo Uganda kushika mkia.
Mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu za Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda na Malawi yamemalizika kwa mafanikio makubwa huku lengo likiwa ni kukuza mchezo huo hapa nchini.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni