
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangalla jana Desemba 8,2017 Mjini
Dodoma, ameunda kamati ya kuongoza maandalizi ya namna watanzania na
wageni wa Tanzania watakavyosherehekea Utanzania wao kwenye mwezi
maalum utakaojulikana kama ‘TANZANIA HERITAGE MONTH’.
Akielezea
wakati wa kutangaza kamati hiyo iliyojumlisha wadau mbalimbali wakiwemo
wanahabari, wanamichezo na wadau wengine mbalimbali na wafanyabishara,
alisema:
“Kwenye
mwezi huu kila kitu kitakuwa cha kitanzania na tutataka kwenye kila
ofisi ya umma, ofisi binafsi, shule, chuo, hotel, balozi zetu n.k mtu
akifika tu, ‘utanzania’ wetu uonekane!” alieleza Dk.Kigwangalla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni