Wanaharakati nchini India wameandamana kushinikiza watu waliofungwa kwa makosa ya ubakaji kunyongwa haraka. Wabakaji wa watoto wanapaswa kuuawa katika muda wa miezi sita tangu watekeleza uovu huo, mteteaji mkuu wa haki za wanawake India amependekeza.
liongozwa na Mtetezi wa Haki za Wanawake nchini humo, Swati Maliwal.
Bi Maliwal ameliambia gazeti la Hindu Times kuwa amepeleka barua ya maombi hayo kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi.
Maandamano hayo yalifanyika ikiwa ni kumbukumbu ya miaka mitano tangu mwanafunzi wa chuo cha Afya, Jyoti Singh ( 23) alipobakwa na kundi la wanaume hadi kufa.
“Hakuna kilichobadilika katika miaka mitano iliyopita kwani vitendo vya ubakaji bado vinaongezeka nchini. New Delhi bado ndio mji unaoongoza kwa vitendo vya ubakaji. Mwezi uliopita, mtoto wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa na kundi la wanaume, na ubakaji wa mtoto wa miaka saba,na mwingine wa kike wa mwaka mmoja na nusu alibakwa.“amesema Swati Maliwal kwenye mahojiano yake na BBC.
Imeelezwa kuwa mjini Delhi watoto watatu wa kike kuanzia umri wa miaka 2-10 hubaka huku wanawake 6 wenye umri kati ya miaka 18-25 hubakwa na kunyanyasa kingono.
India ilifanyia mabadiliko katika sheria zake kuhusu ubakaji baada ya kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na unyanyasaji kingono ambapo ilichukua hatua kuharakisha kusikilizwa kwa kesi hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni