
Patashika ya michuano ya #CECAFA2017 kufikia tamati leo kwa fainali na mechi ya mshindi wa tatu kupigwa na mechi zote zitakuwa Live Azam Sports 2.
Burundi kukipiga na Uganda katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu, saa 7:30 mchana, Mechi hii itakuwa ni marudio ya mechi ya Desemba 4, 2017 ambapo timu hizi zilikutana katika mechi ya kwanza ya Kundi B na kutoka sare tasa ya 0 - 0 je leo nani kuibuka mbabe.
Na fainali ni Zanzibar Heroes dhidi ya Kenya mechi hii itakuwa inakumbushia mechi ya Desemba 9, 2017 ambapo timu hizi zilikutana na kutoka sare tasa 0 - 0, Je leo nani kuwa bingwa?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni