Jumapili, 31 Desemba 2017

TFF latoa onyo kali


 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa onyo kali na kulaani vitendo vyovyote vya kuwabugudhi au kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao katika mashindano yote yaliyochini ya TFF.

''Tunalaani vitendo vyovyote vya kuwabugudhi au kuwazuia waandishi wa habari kufanya kazi zao katika utaratibu tuliojiwekea'', imeeleza taarifa ya TFF.

TFF pia imetoa onyo kali huku ikiahidi kuwachukulia hatua wahusika waliosababisha kukwamisha shughuli za wanahabari kwenye michezo ya Ligi daraja la kwanza kati ya Dodoma FC dhidi ya Alliance pamoja na Biashara dhidi ya Pamba FC.

Shirikisho hilolimeongeza kuwa litaendelea kushirikiana na Vyombo vya habari kwasababu wanaamini katika Uhuru wa Habari.

''Vyombo vya habari ni moja ya wadau muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu ambao siku zote tunashirikiana nao na tutaendelea kushirikiana nao''. imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni