mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumapili, 31 Desemba 2017
BREAK NEWS; Askofu Kakobe azungumzia utajiri wake
kiwa yamebaki Masaa machache kabla ya mwaka 2017 kumalizika na kuukaribisha mwaka mpya wa 2018, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe ameunguruma katika ibada aliyoiongoza Leo kanisani huku akijinasibu kuwa ni Tajiri kuliko Serikali zote duniani
Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zacharia Kakobe amesema kwamba yeye sio tu Tajiri kuliko Serikali ya Tanzania, Bali ni Tajiri kuliko Serikali zote duniani ikiwemo ya Marekani na Uingereza'.
" Wanaosema Kakobe amekimbia nchi nawashangaa sana sipo na wala siendi popote, kipindi Fulani walikuja kuchunguza uraia wangu lakini wakaambulia patupu, tutabanana hapa hapa" Askofu Kakobe
" Watu wanasema Niko kimya sana wala sipo kimya tatizo wanataka nizungumze wanayoyataka wao, sasa Mimi sio mtu wa namna hiyo, ukiniona nimesimama katika madhabau Hays basi ujue nina kibali cha Mungu, mtu ukitwa Mbwa kwani wewe ndio itakua Mbwa? Sasa nashangaa unaogopa nini kuitwa Mbwa wakati wewe sio Mbwa" Askofu Kakobe
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni