
Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosimama kupisha michuano ya kombe la #CECAFA2017 inaendelea mwishoni mwa mwezi huu kwa mechi za raundi ya 12 zitakazochezwa kati ya Desemba 29 mwaka huu na Januari mosi mwakani.
Taaraifa ya bodi ya ligi iliyotolewa leo imeeleza kuwa mechi 16 kati ya 152 zilizobaki za ligi hiyo zitachezwa kuanzia saa 8:00 mchana kwa kuwa kanuni zinaruhusu.
Kwa mujibu wa bodi ya ligi, uamuzi huo umefanywa ili kuongeza mechi ambazo zinataoneshwa moja kwa moja (live) na mdhamini wa matangazo (Azam TV), hatua ambayo itaisaidia kufuatilia kwa karibu uchezeshaji wa waamuzi na pia kutoa nafasi kwa wadhamini wa ligi pamoja na wa klabu kuonekana zaidi (mileage).
Ratiba yenyewe iko hivi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni