
Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema CHADEMA wamefanya kikao cha dharura kususia uchaguzi wa marudio kwa majimbo na kata.
Katika
kikao hicho, Polepole anadai CHADEMA wanatumia mgongo wa kuminywa kwa
Demokrasia nchini kususia uchaguzi huo wakati ukweli ni kwamba wamefulia
baada ya kutumia vibaya hela ya mfuko wa chama chao.
"Watani
wanakutana leo, agenda ni kutoshiriki uchaguzi unaokuja wa marudio kwa
kisingizio cha demokrasia lakini ukweli ni matumizi mabaya ya fedha
yamefuja mfuko wa chama. Tafuteni visingizio vingine lakini sio
demokrasia. Watu wamechoka siasa za matukio. Kikao chema!" Ameandika polepole katika ukurasa wake wa Twitter.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni