Jumatano, 6 Desemba 2017

Patashika ya michuano ya #CECAFA kuendelea kushika kasi kesho Alhamisi December 07..


Patashika ya michuano ya #CECAFA kuendelea kushika kasi kesho Alhamisi December 07..

Saa 8:00 mchana ni vita ya ndugu wawili Tanzania Bara "Kilimanajro Stars" dhidi ya 'Zanzibar Heroes', mechi hii itakuwa inakumbusha mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu katika michuano ya CECAFA 2012, ambapo Zanzibar Heroes waliibuka washindi wa tatu baada ya kuibamiza Kilimanjaro Stars kwa mikwaju ya penati 5 - 6 baada ya dakika 90' kuisha kwa sare ya 1-1.
Je kesho nini kitatokea, majibu yatakuwa #AzamSports2 itakuletea Live mchezo huu

Wakati mpambano kati ya Ethiopia na Burundi,utakuwa Live #AzamONE saa 9:00 Alasiri

Baada ya Rwanda kuchezea kichapo katika mechi mbili za kwanza, atashuka tena dimbani kuumana na Libya, je atakubali kuchezea kichapo tena? #AzamSports2 itakupa kila kitu Saa 10:00 jioni.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni