Kiungo
mchezeshaji wa Simba Mnyarwanda, Haruna Niyonzima amesema kati ya
washambuliaji wanaotajwa kutua Simba, Ismaila Diara raia wa Mali ndiye
anayestahili kuichezea timu hiyo
Diara
anayeichezea Rayon Sports ni kati ya wachezaji wanaotajwa kutua Simba
pamoja na Nahimana Shasir kutoka Rayon na Elias Maguli aliye na kikosi
cha Kilimanjaro Stars kinachoshiriki Chalenji nchini Nairobi, Kenya.
Washambuliaji
hao, wamepangwa kuongezwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo
lililofunguliwa Novemba 15, kabla ya kufungwa Desemba15, mwaka huu.
Niyonzima amesema anawafahamu uwezo wa wachezaji wote wa Rwanda, lakini anafurahishwa na uwezo wale wa kufunga mabao Diara.
Niyonzima
alisema, sifa yake nyingine aliyokuwa nayo mshambuliaji huyo ni uzoefu,
umbile kubwa na nguvu alizonazo za kupambana na mabeki wakorofi wa timu
pinzani.
“Kwanza
nikwambie kitu kimoja, ligi kuu ya hapa nchini ni ngumu na ina
ushindani mkubwa na changamoto nyingi, hivyo basi ni lazima umakini uwe
mkubwa katika kusajili wachezaji.
“Mimi
binafsi ninavutiwa na aina ya uchezaji wa mshambuliaji wa Rayon ambaye
hivi sasa ndiye anayetegemewa katika timu yake kwa ajili ya kufunga
mabao.
“Mshambuliaji
huyo ndiyo kwanza kujiunga na timu msimu wake wa kwanza, lakini kama
viongozi wakifanikisha usajili wake, basi tutakuwa tumelamba dume kwani
ni mshambuliaji mwenye sifa zote tofauti na uzoefu wake wa mashindano ya
kimataifa,”alisema Niyonzima.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni