Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amezua gumzo mitandaoni baada ya kubadilisha staili yake ya kufunga nywele kwa nyuma na kunyoa kipara.
Muonekano mpya wa Drogba.
Mpaka sasa hivi picha hiyo aliyoiweka jana imepata likes, comments na Retweets zaidi ya elfu 1 kwenye mtandao wa Twitter.
Drogba ambaye kwa sasa anakipiga kunako Ligi kuu Soka Marekani katika klabu ya Phoenix Rising FC amekuwa moja ya wachezaji wakukumbukwa katika klabu ya Chelsea kwa muda wote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni