Ijumaa, 3 Novemba 2017

Yanga SC, Simba SC na Azam FC kuzisaka pointi tatu muhimu wikiendi hii



Ligi Kuu soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea wikendi hii kwa michezo mitano  kuchezwa kwenye  viwanja mbalimbali hapa nchini

ingida United ikiwa katika Uwanja wake wa Namfua itaikaribisha Yanga SC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kagera Sugar watakuwa wenyeji huko Bukoba katika dimba la Kaitaba watakapo wakaribisha Tanzania Prisons.
Njombe Mji wakiwa nyumbani katika dimba la Sabasaba Njombe watawakaribisha Mbao FC.
Azam FC itashuka katika Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es salaam kucheza na Ruvu Shooting.
Ndanda FC wakiwa mkoani Mtwara  watashuka katika Uwanja wa Nangwanda kucheza na Mtibwa Sugar.
Na hapo keshokutwa siku ya Jumapili ya Novemba 5 timu ya Lipuli FC ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani wa Samora mkoani Iringa itashuka dimbani kumenyana na Mwadui FC wakati Mbeya City itakuwa Sokoine Mbeya kuwakabili vinara wa ligi klabu ya Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni