Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wanatoa misaada na makazi kwa wakimbizi wa Rohingya ambao waliwasili Bangladesh. Wamesema wakimbizi 3,000 waliwasili katika mpaka wa Anjuman Para kati ya Jumatano na Alhamisi asubuhi wiki hii.
UNHCR inasema pindi wakimbizi wanapowasili wanaelekezwa katika kambi ya Kutupalong ambako wanapokea huduma mbali mbali ikiwemo huduma za afya, chakula, maji na mahitaji ya msingi.
Kamishina mkuu msaidizi wa masuala ya wa ulinzi wa UNHCR ambaye amemaliza ziara yake Myanmar amerejelea wito wa Umoja wa Mataifa kuhusu ufikiaji wa raia katika jimbo la Rakhine na haki ya wakimbizi kuweza kurejea nyumbani. Babar Baloch ni msemaji wa UNHCR
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni