
Baada ya ziara yake katika mikoa ya Katavi na Rukwa, kikosi cha kikosi cha klabu ya Simba ambao ni vinara wa VPL, kinarejea leo jijini Mbeya kuendelea na kambi ya maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Prisons.
Simba ilicheza mechi ya kirafiki siku ya Jumanne dhidi ya timu ya Nyundo
FC ya mkoani Katavi ambapo timu hizo ziLitoka sare ya bila kufungana.
Mchezo huo ulipigwa kwenye dimba la Azimio mkoani humo.
Baada ya mchezo huo Simba ilisafiri hadi mkoani Rukwa ambapo jana jioni
ilishuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Rukwa Stars.
Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 3-1.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo inaeleza kuwa kikosi hicho
kinarejea jijini Mbeya kwaajili ya kuendelea na kambi ya maandalizi ya
mchezo wake wa ligi kuu raundi ya 11 dhidi ya Tanzania Prisons
utakaopigwa Novemba 19.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni