
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam imeandaa sherehe maalum ya pamoja kwaajili ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vyote vya elimu ya juu vya mkoa wa Dar es salaam.
Sherehe hiyo itakayogharamiwa na ofisi hiyo, inatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii (Desemba 2, 2017) katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kuelekea katika tukio hilo kubwa na la kwanza kufanyika mkoani humo, leo kamati ya maandalizi ya inayoundwa na marais wa vyuo vyote chini ya mwenyekiti wao Lecton Leskar Moris kutoka chuo kikuu cha Hubert Kairuki, leo wametembelea baadhi ya maeneo patakapofanyika tukio hilo.
Pia kamati hiyo iliyoambatana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akiwa na wakili Albert Msando imepata fursa ya kutembelea maduka yaliyopo katika eneo la Mlimani City.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni