
Baada ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta kwenye uwanja wa Kasarani, wafuasi wa NASA wamezusha ghasia na kuchoma magari, maduka na baadhi ya maeneo ya biashara katika maeneo ya Barabara ya Manyanja, Nairobi.
Polisi nchini humo wanadaiwa kupambana na wafuasi hao ambapo mabomu ya machozi na risasi zimesikika zikirindima huku polisi hao wakiwa wametanda mitaani wakijaribu kuwatawanya.
Hatua hiyo imekuja baada ya wafuasi hao kuzuiwa kuendesha ibada ya kuwakumbuka wafuasi wao waliokufa katika machafuko ya kisiasa baada ya chaguzi zote mbili, iliyokuwa ifanyike kwenye viwanja vya Jacaranda, Embakasi.
Wakati huo huo. Kiongozi wa NASA, Raila Odinga amesema, ataapishwa kuwa rais Desemba 12



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni