Jumatano, 8 Novemba 2017

Kupiga picha Daraja la Nyerere Tsh. 250,000






Ili kuhakikisha usalama katika Daraja la Nyerere, Kigamboni kwa wale wanaokwenda kwa ajili ya kupiga picha serikali imetoa utaratibu maalumu.
 Kwa sasa watu wanaokwenda kupiga picha katika daraja hilo watalazimika kulipia gharama kwa ajili ya usalama wa watumiaji wa barabara, fedha zinazokusanywa, wapiga picha wenyewe pamoja na kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Gharama za upigaji picha kwa matukio maalumu (harusi, kwaya, wasanii) ni Tsh 250,000 kwa saa moja. Wanaopiga picha moja moja (selfie) hawatolipa, lakini wametakiwa kuchukua tahadhari ya usalama wao.
Hata hivyo wapiga picha watalazimikakuomba kibali kwenye Ofisi Mkurugenzi Mkuu ambapo pia watapatiwa maelezo ya kufuata.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni