Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco jana usiku imeibuka bingwa mpya wa bara la Afrika kwa upande wa soka ngazi ya Klabu baada ya kuifunga Al Ahly ya Misri bao 1-0 kwenye fainali ya pili ya klabu bingwa barani Afrika. Na kufuzu moja kwa moja kwenye michuano ya Kombe la Dunia la Vilabu ambapo wameungana na mabingwa wa Ulaya, Real Madrid.
Bao la ushindi la Wydad Casablanca lilifungwa na El Karti kipindi cha pili na kufanya matokeo ya jumla katika mechi zote mbili kuwa 2-1, baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 wiki mbili zilizopita nchini Misri.
Ubingwa huo kwa Wydad unakuwa wa pili tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo ambapo mara ya kwanza kutwaa ilikuwa ni mwaka 1992.
Wydad sasa itaiwakilisha Afrika kwenye michuano ya kombe la dunia la vilabu mwezi Desemba mwaka huu. Michuano hiyo itafanyika katika nchi za falme za kiarabu (UAE) ambapo wataungana na timu nyingine kutoka kwenye mabara mengine ikiwemo mabingwa wa Ulaya klabu ya Real Madrid.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni