mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumatano, 29 Novemba 2017
“Ipo siku nitakufa, hakuna anayeishi milele” – WEMA SEPETU
2017 muigizaji kutokea Bongomovie Wema Sepetu ameamua kuandika dukuduku lake kuhusiana na matusi ambayo amekuwa akitukwana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo limemfanya aseme anatamani kutokuendelea kuwepo kwenye mitandao hiyo.
Wema ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe huo na kuonesha jinsi gani amechoshwa na hali hiyo. Kwenye akaunti yake hiyo Wema ameandika….>>>”Ipo siku nitakufa, hakuna anaeishi milele… Sijui mtaendelea kunisema kwa kejeli na kunitukana matusi ya nguoni au ndo itakuwa, “Maskini ya Mungu, Dada wa watu alikuwa hivi na vile, Mungu ailaze Roho yake mahali pema…” Kuna muda mwingine huwa natamani Allah Subhannah wata’allah anichukue tu…
“Ya Duniya ni mengi sana…. Kuna muda mwingine nakufuru mwenyezi Mungu na kutamani labda hata nisinge exist… Ila acha niendelee kumtegemea yeye… Kila jambo hutokea kwa sababu…. Hili nalo litapita… I think I need a Time Off Social Media… Kwa mara nyingine Tena…. Siwezi jamani…” – Wema Sepetu
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni