Jumatano, 29 Novemba 2017

Akata nyeti za Mwanae kwa madai yakufukuza Mapepo mabaya



 MTU mmoja huko mwenye umri wa miaka 39 huko Chhattisgarh, India, amemtoa kafara mwanaye mdogo katika kitendo cha ushirikiana kwa kumkata uume na sehemu za kichwa kwa shoka hadi kusababisha kifo chake, kwa madai ya kufukuza mapepo mabaya ‘mashetani’.




 Kitendo hicho kilifanyika huko Balodabazar wilayani Chhattisgarh, polisi walisema jana. Ramgopal Patel, na mganga wa kienyeji, Rajesh Yadav (19) walikamatwa leo, ikiwa ni siku mbili baada ya kufanya kitendo hicho kijijini Amera.

Polisi walisema mwili wa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 ulikutwa ukiwa katika dimbwi la damu ambapo baada ya polisi kufanya uchunguzi, Patel alikiri kumwua mwanaye huyo ili kuondoa mapepo mabaya na hivyo wamemfungulia mashitaka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni