Ijumaa, 3 Novemba 2017

FAO yachapisha kitabu cha mienendo ya uhamiaji vijijini


 hirika la chakula na kilimo duniani, FAO leo kimechapisha kitabu cha ramani kinachorahisisha uelewa wa mwenenendo wa uhamiaji kwenye maeneo ya vijijini katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.
Mkurugenzi Mkuu msaidizi wa FAO anayehusika na masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii Kostas Stamoulis amesema hatua hiyo ni kwa kuzingatia kuwa ifikapo mwaka 2030 idadi kubwa ya nguvukazi itakuwa vijijini hivyo ni lazima ifahamike watakuwepo maeneo yapi.
Kitabu hicho kinadokeza katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, watu wanahamia nchi jirani, kikitolea mfano Kenya na Senegal ambapo nusu ya wahamiaji wake wanakwenda nchi jirani.
Kitabu pia kinaangazia dhima muhimu ambayo maeneo ya vijijini yatakuwa nayo katika kubadili mwenenendo wa uhamiaji barani Afrika katika miongo ijayo.
Kwa mujibu wa Bwana Stamoulis ongezeko la idadi ya watu linamaanisha ongezeko la nguvukazi na hivyo ifikapo mwaka 2030 kutakuwepo na watu wapatao milioni 380 wenye uwezo wa kufanya kazi na kati yao hao milioni 220 watakuwa vijijini.
Kwa mantiki hiyo watunga sera wanapaswa kuzingatia mienendeo hiyo ili kuhakikisha kilimo na maendeleo vinaangaziwa katika mipango yote ya mienendo ya uhamiaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni