Jumatatu, 27 Novemba 2017

Beyonce kutumbuiza kwa dau hili kwenye harusi ya Gareth Bale








Mwanamuziki maarufu duniani kutoka nchini Marekani, Beyonce huenda akawa mtumbuizaji kwenye harusi ya mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale.






Ripoti kutoka kwa watu wa karibu na familia ya Bale wamesema familia yake ipo kwenye mazungumzo na Mwanamuziki huyo wa Pop duniani.
Gazeti la The Sun la Uingereza limeripoti kuwa Beyonce anataka kiasi cha Euro milioni £1.5 sawa na Tsh bilioni 4 ili kutumbuiza kwenye party maalumu kwenye harusi hiyo.
Gareth Bale anatarajia kufunga ndoa mwaka ujao na mzazi mwenzake, Emma Rhys-Jones ambaye wamezaa nae watoto wawili na tayari wawili hao mwezi ujao wamepanga kwenda Italia kufanya tafrija ya kifamilia na baadhi ya marafiki zake kutoka nchini Wales. Beyonce pia ametajwa kuhudhuria kwenye party hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni