Jana jumapili usiku kulikuwa na mechi kubwa nchini Hispania ambapo miamba ya La Liga, Barcelona na Valencia ilikutana kwenye mchezo wa Ligi.
Mechi hiyo ilianza kwa kasi kipidi cha kwanza ambapo klabu ya Barcelona ilimiliki mpira kwa asilimia 71 kwa 29 dhidi ya Valencia lakini hiyo haikuwasaidia kwani hadi kipindi cha kwanza kinaisha matokeo yalikuwa 0-0.
Gumzo kubwa kwenye kipindi hicho cha kwanza ni pale Mpira mrefu aliyoupiga mshambuliaji Lionel Messi kumshinda nguvu mlinda mlango wa Valencia, Neto Murara na kumponyoka na kuvuka mstari kabla ya golikipa kuutoa nje mpira huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Barcelona kutokea kwa tukio kama hilo kwani msimu uliopita pia walipatwa na janga kama hilo kwenye mchezo dhidi ya Real Betis ambapo mpira uliingia kabisa kwenye nyavu lakini refa alikataa goli hilo.
Mechi hiyo ya jana Barcelona walichomoa goli dakika ya 82 kupitia kwa beki wao wa kushoto Jordi Alba hii ni baada ya mshambuliaji wa Valencia, Rodrigo kuwazidi ujanja mabeki wa Barcelona na kupachika goli kunako dakika ya 72.
Mchezo huo ambao ulifanyika kunako dimba la Estadio Mestalla ulikuwa ni wa 11 kwa Klabu ya Barcelona kupata angalau pointi kwani mara ya mwisho kufungwa uwanjani hapo ilikuwa ni Februari 18 mwaka 2007 ambapo Barca walifungwa goli 2-1.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni