Jumatano, 11 Oktoba 2017

Siku ya mtoto wa kike duniani yaadhimishwa leo






Leo ni siku ya mtoto wa Kike duniani ambapo ujumbe unajikita kwenye kuwezesha mtoto wa kike kabla, wakati na baada ya majanga.
Umoja wa Mataifa unasema ujumbe huu unaangazia watoto wa kike bilioni 1.1  duniani kote ambao ni chanzo cha ari, ubunifu na uthabiti.
Ujumbe pia unaangazia mamilioni ya watoto hao ambao wamenasa kwenye majanga ambapo katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF jijini New York, Marekani kunafanyika tukio maalum la kuweka mazingira bora ya kumaliza ukatili dhidi ya watoto wa Kike.
Hata hivyo nchini Uganda, wakati wakisubiri harakati za kuwalinda, watoto wenyewe wa kike wamechukua
 hatua kujilinda dhidi ya ukatili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni