Ijumaa, 27 Oktoba 2017

Polepole awatahadharisha wanaotaka kuhamia CCM



Katibu wa Itikadi na wa na Uenezi CCM Taifa, Ndg. Humphrey Polepole amewatahadharisha watu wanaotaka kujiunga ndani ya Chama Cha mapinduzi kwa kudhani kwamba kuna namna rahisi ya kupata pesa asiende ndani ya Chama hicho kwa sasa.

Akifanya mahojiano maalumu na East Africa Tv, Polepole amesema kwamba  mambo ambayo yanatajwa na kuhusishwa kwenye CCM kama Rushwa na ununuzi wa madiwani hayana nafasi ndani ya chama chao kwani havina mashiko kwani ni kinyume na misingi pamoja na imani ya chama hicho hivyo watu wasijipe imani kuhamia huko wakidhani watapata nafasi.

Polepole amesema kwamba anafahamu kwamba wapo viongozi wengi sana wanaotaka kuingia kwenye chama cha mapinduzi kuliko hata wale ambao tayari wamekwisha pokelewa na hiyo ni kwa sababu chini ya uongozi wa awamu ya tano wameweza kufikia matarajio na yale ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele.

"Waliokuja CCM ni wachache mno. Bado wapo viongozi wengi sana ambao wapenda kuja kwenye chama chetu, nikiri ni wengio kuliko ambao tumewapa ridhaa. 

"Wengi ambao wanaomba kurejea kwenye chama cha mapinduzi ni wale waliokuwa tofauti na CCM lakini kinachofanya na ndugu yetu Magufuli ndicho walichokuwa wakitaka kukiona kwa muda mrefu..... 

"Watu wengi waliamini CCM ni ileile ni kweli  lakini ni ilele imekuwa chama ambacho kinaongozwa katika misingi ambayo ipo kwenye katiba...." Amesema Polepole

Polepole amesema kwamba kwa sasa CCM imejikita kuwa chama cha wanachama wenyewe na siyo kuwa kikundi cha watu ambacho kinatatua matatizo ya watanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni