
August 11, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali maombi ya Bodi
ya CUF inayomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif ya kutaka Msajili wa
Vyama vya Siasa asitoe ruzuku kwa CUF upande wa Profesa Ibrahim Lipumba.
Maombi hayo namba 21 ya mwaka 2017 yametupiliwa mbali na Jaji Wilfred
Dyansobera, baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata
anayemuwakilisha mdaiwa wa pili Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kusema
kesi imeitishwa kwa ajili ya uamuzi.
Katika uamuzi maombi hayo ambayo mdaiwa wa kwanza ni Prof. Lipumba, Jaji
Dyansobera amesema anakubaliana na moja kati ya pingamizi la AG kwamba
vifungu vya sheria vilivyotumika kufungua shauri hilo sio sahihi.
Hata hivyo, amesema anakubaliana na hoja za Bodi hiyo iliyo upande wa
Maalim Seif kwamba suala la Bodi hiyo kutokuwa na uhalali linahitaji
ushahidi wa kina.
Aidha, kuhusu suala la Maalim Seif kusaini hati mbalimbali za shauri
hilo bila kupewa mamlaka, amesema hilo sio pingamizi kwani Mahakama
haiwezi kutoa uamuzi kwa kuangalia kiapo tu.
>>>”Hivyo mahakama imetupilia mbali maombi hayo, kwa sababu
sheria iliyotumiwa kufungua maombi hayo sio sahihi, lakini waombaji
wanaweza kukata rufaa ama kufungua kesi nyingine.”
Baada ya kuelezwa hayo, upande wa Maalim wamesema watafungua upya kesi hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni