
Japan imepeleka mtambo wa kutibua
makombora magharibi mwa taifa hilo kufuatia tishio la Korea Kaskazini
kwamba itarusha kombora la masafa marefu katika kisiwa cha Guam nchini
Marekani.
Mtambo huo kwa Jina PAC3 (Patriot Advanced Capability-3)
umepelekwa katika eneo la shimane, Hiroshima na Kochi ambapo Pyongyang
inasema kombora lake litapaa kabla ya kuanguka katika maji ya Guam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni