Jumamosi, 12 Agosti 2017

Alichozungumza Uhuru kuhusu Odinga baada ya kutangazwa mshindi




Muda mfupi baada ya kutangazwa mshinda na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika Jumanne August 8, 2017 kwa kupata kura 8,203,290 dhidi ya kura 6,762,224 za Raila Odinga, Uhuru Kenyatta amempongeza mpinzani wake huyo.
Kenyatta ambaye anarudi kwenye uongozi kwa muhula wa pili amempongeza mgombea Raila Odinga akisema katika kila mashindano lazima apatikane mshindi na aliyeshindwa huku akisisitiza umoja ili kuijenga Kenya huku akiahidi kuwahudumia Wakenya wote waliomchagua na wasiomchagua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni