mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumanne, 22 Agosti 2017
Alichojibu Polepole baada ya kuambiwa viatu vya Nape vinampwaya
Kupitia kwenye account yake ya twitter Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’ Humphrey Polepole ametoa majibu kwa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akimwambia kuwa hatokuwa tena Mbunge baada ya Awamu hii.
Hatua hiyo ya Polepole imekuja baada ya kuambiwa na Mbunge Msigwa kuwa viatu vya Nape havimtoshi kupitia twitter ambapo aliandika>>>”Kitendo cha Msukuma kumkumbuka Nape , ni ujumbe tosha Kuwa Viatu vya Nape vinampwaya POLEPOLE!”
Baada ya ujumbe huo naye Polepole kupitia twitter aliandika>>>”Kitu kimoja nakuahidi, hii ni term yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona mchungaji anajichanganya na mbuzi.”
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni