Alhamisi, 13 Julai 2017

Ulemavu sio kulemaa tunachotaka ni kuwezeshwa




Kuwa mlemavu haimanishi huwezi kushirikishwa katika maendeleo ya jamii na hasa katika umimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDG's.
Hayo yamesemwa na Rebecca Altsi kutoka shirika la kimataifa la IF linalojihusisha na walemavu wa mgongo wazi na wenye vichwa vikubwa Afrika ya Mashariki na Bi Fatma Wangari kutoka shirika la kimataifa la inclusion Africa linalohusika na walemavu wa akili.
Wako hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhuduria mkutano unaotathimini hatua zilizopigwa katika utekelezaji wa SDGs.
Rebecca ambaye ni mlemavu anayetumia kitimwendo anasema katika utimizaji wa SDG's kuna hatua ya kumtambua mlemavu lakini changamoto ni katika sera na utekelezaji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni