
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
imewaachisha kazi wafanyakazi 12 waliokuwa wamesimamishwa kwa mwaka
mmoja sasa.
Wafanyakazi hao walisimamishwa kazi Julai 2016 kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi.
Taarifa ya NSSF iliyotolewa leo Alhamisi (Julai 13) kupitia vyombo vya
habari walioachishwa kazi ni Yacob Kidula, aliyekuwa mkurugenzi wa
mipango, uwekezaji na miradi.
Wengine na nafasi walizokuwa wakishikilia kwenye mabano ni Ludocick
Mrosso (mkurugenzi wa fedha), Chiku Matessa (mkurugenzi wa rasilimali
watu na utawala), Sadi Shemliwa (mkurugenzi wa udhibiti, hadhara na
majanga), Pauline Mtunda (mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za ndani).
Crescentius Magori (mkurugenzi wa uendeshaji), Amina Abdallah (meneja
utawala), Abdallah Mselli (meneja wa uwekezaji), Mhandisi John Ndazi
(meneja miradi), Wakili Chedrick Komba (meneja kiongozi Mkoa wa Temeke)
na Ramadhani Nassibu (meneja mkuu usalama).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni