aziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema ujio wa timu ya Everton nchini utaweza kufungua fursa nyingi kwa kuwa dunia nzima sasa itaitazama Tanzania kupitia mchezo kirafiki dhidi ya Gor Mahia.
Mwakyembe amebainisha hayo muda mchache alipoupokea ugeni huo huku
akizisisitizia timu za Tanzania kutumia viwanja vilivyopo nchini vizuri
ili waweze kuinua vipaji kwa hali ya juu.
"Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kwanza kuwaona hawa nyota wa Everton
ni timu kongwe kutoka Uingereza lakini pili inafungua fursa sana maana
inatutangaza watanzania kidunia, wamekuja na watangazaji kutoka nchi
mbalimbali. Kwa hiyo inafungua milango kwa timu nyingi zaidi, nasi
tuzishawishi zaidi timu zetu zije kutumia viwanja vyetu vya kisasa
tulivyo navyo", amesema Mwakyembe.
Pamoja na hayo, Mwakyembe amewatuliza wanahabari pamoja na wapenzi wa
soka kuwa na moyo wa uvumilivu kwa kuwa hawataweza kupata nafasi ya
kukiona kikosi hicho kikiwa kinafanya mazoezi yake kwa ajili ya mchezo
wa kesho dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kutokana na kuwepo na ulinzi mkali.
"Nafikiri kesho kutakuwa na mchezo mzuri kweli, leo watafanya mazoezi
katika uwanja Taifa lakini naona wenzetu hawataki kabisa kuona vyombo
vya habari pale, hatuwezi kuwapinga kwa hilo. Kwa hiyo vijana wangu
msihangaike hata kwenda pale maana kuna ulinzi mkali lakini kesho
nitahakikisha kila mmoja wenu anapata nafasi nzuri kuweza kufuatilia
mchezo huo jioni", amesisitiza Mwakyembe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni