Muigizaji Johnny Depp amemuangukia na kumuomba radhi Rais wa Marekani Dolnad Trump kwa maneno aliyomtolea akiwa katika jukwaa la sherehe za Glastonbury.
Depp alitoa maneno yenye kuashiria kumchukia Rais huyo,kwa kuuliza ni lini ilikuwa mara ya mwisho kwa muigizaji kumuua rais wa Marekani jambo lililotafsiriwa kuwa ni kumchukia Rais Trump ambaye ameingia madarakani mwaka jana, hata hivyo muigizaji huyo ameamua kufuta maneno yake na kuonesha kumuomba radhi kwa kupiga magoti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni