Jumamosi, 27 Januari 2018

Dakika 85': #VPL Mwadui FC 2-2 Njombe Mji.

Image may contain: text

#VPL Gadiel Michael katika uwanja ambao umemlea, anatandika fataki la mbali kabisa na kuipa Yanga bao la pili dakika ya 44. Azam 1-2 Yanga.

Image may contain: text

#VPL Obrey Chirwa anaisawazishia Yanga, mambo yanazidi kunoga kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi, Azam 1-1 Yanga

No automatic alt text available.

Mume amteka mkewe, aamuru rafiki yake ambake kisha kammwagia tindikali…..kisa?

Binti wa miaka 24 mwenye mtoto mmoja ambaye ni raia wa Kenya, ameuawa kikatili baada ya kutekwa na mume wake ambaye alikuwa na rafiki yake kisha kumwambia rafiki yake huyo ambake binti huyo na baada ya mateso hayo kwa kushirikiana wakamwagia tindikali.
Lucy Ndungu aliwekewa dawa za kulevya na mumewe na ndipo alipoweza kumteka akiwa na rafiki yake, na baada ya kumbaka na kummwagia tindikali waliutupa mwili wake kando ya barabara.
Familia ya marehemu imeeleza kuwa ilimkuta Lucy anamajeraha ya kuungua kwa 75% ya mwili mzima huku hali yake ikiwa mbaya sana na hivyo akawahishwa katika Hospitali ya Taifa Kenyatta kupatiwa matibabu lakini hata hivyo akiwa kwenye matibabu hayo alifariki dunia.
Inaelezwa sababu ya mume huyo kufanya hivyo ni kwamba, walikuwa kwenye ugomvi na Lucy akaamua kuachana naye na kuondoka nyumba waliokuwa wanaishi pamoja na kukataa kurudiana na mumewe huyo jambo ambalo linadaiwa kumkasirisha mwanaume huyo.

DAKIKA 4 AZAM WANAANDIKA GOLI AZAM 1 YANGA 0


KIPUTE KARIBIA KUANZA!!

Image may contain: one or more people, outdoor and text

NEC YATOA MAAMUZI MAZITO RUFAA YA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI: Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo ya kuruhusu mgombea wa chadema kuendelea kuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Kinondoni. Yatoa pia maamuzi juu ya rufaa tano za wagombea udiwani

Image may contain: text

Hizi hapa mechi zitakazopigwa leo katika #VPL

No automatic alt text available.

MRADI WA CHUO CHA VETA LUDEWA WANUKA RUSHWA, MENEJA MRADI ASIMAMISHWA:

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof Joyce Ndalichako imeitaka mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi katika mradi wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi VETA kilichopo wilayani Ludewa mkoani Njombe kutokana na ujenzi wa chuo hicho kuhusishwa na vitendo vya rushwa.

“Ninaiagiza bodi ya VETA kumsimamisha kazi meneja miradi wa VETA Denis Masoi kwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi isiyo na sifa. Meneja huyu amekuwa akinidanganya kwamba mradi unaendelea vizuri…ni kipi kizuri kinaendela hapa.”

“Ninaitaka bodi pia ifike eneo la mradi…wakae na mshauri elekezi na ndani ya wiki moja waniletee ushauri wa namna gani mradi huu unaweza kujengwa kwa muda mfupi,” alisema Ndalichako.

Awali waziri Ndalichako ametembelea katika chuo cha ufundi stadi kilichopo Makete na kuwataka wakala wa majengo hapa nchini kujitathmini kwa kushindwa kutii mkataba waliokubaliana na serikali na kuchelewesha ujenzi tofauti na makubaliano ya mkataba .




#VPL VIKOSI: AZAM FC VS YANGA SC LEO


Kikosi cha Azam FC: Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Agrey Moris, Yakubu Mohamed, Stephan Kingue, Joseph Kimwaga, Salum Abubakar, Bernard Arthur, Shabani Chilunda, Enock Atta.

Mwadini Ali, David Mwantika, Abdallah Kheri, Salmin Hoza, Idd Kipagwile, Mbaraka Yusuph, Paul Peter

Kikosi cha Yanga: Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Said Juma, Raphael Daud, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib, Emmanuel Martin.

SUB: Ramadhan Kabwili, Haji Mwinyi, Edward Maka, Juma Mahadhi, Said Mussa, Matheo Anthony, Geoffrey Mwashiuya.