Jumamosi, 27 Januari 2018

MRADI WA CHUO CHA VETA LUDEWA WANUKA RUSHWA, MENEJA MRADI ASIMAMISHWA:

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Prof Joyce Ndalichako imeitaka mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi katika mradi wa ujenzi wa chuo cha ufundi stadi VETA kilichopo wilayani Ludewa mkoani Njombe kutokana na ujenzi wa chuo hicho kuhusishwa na vitendo vya rushwa.

“Ninaiagiza bodi ya VETA kumsimamisha kazi meneja miradi wa VETA Denis Masoi kwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi isiyo na sifa. Meneja huyu amekuwa akinidanganya kwamba mradi unaendelea vizuri…ni kipi kizuri kinaendela hapa.”

“Ninaitaka bodi pia ifike eneo la mradi…wakae na mshauri elekezi na ndani ya wiki moja waniletee ushauri wa namna gani mradi huu unaweza kujengwa kwa muda mfupi,” alisema Ndalichako.

Awali waziri Ndalichako ametembelea katika chuo cha ufundi stadi kilichopo Makete na kuwataka wakala wa majengo hapa nchini kujitathmini kwa kushindwa kutii mkataba waliokubaliana na serikali na kuchelewesha ujenzi tofauti na makubaliano ya mkataba .




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni