Ijumaa, 21 Julai 2017

Rufaa ya Tigo yagonga mwamba, watakiwa kuwalipa AY na Mwana FA Bilioni 2.1

Image result for FA NA AY IMAGE
 Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na kampuni ya Tigo kupinga kuwalipa wasanii AY na MwanaFA shilingi 2,185,000,000 (zaidi bilioni mbili) kwa kutumia nyimbo za wasanii hao bila kuwalipa.





Wakili wa wasanii hao, Albert Msando amesema huu ni ushindi muhimu kwa sanaa ya Tanzania, kuongeza kuwa “ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria”.
Ikumbukwe kabla ya rufaa ya Tigo, mwaka jana Mahakama Wilaya ya Ilala, iliamuru kampuni ya MIC Tanzania (Tigo) kuwalipa wasanii hao kiasi hicho cha fedha kutumia nyimbo zao bila idhini. Kampuni hiyo ilibainika kutumia nyimbo za wasanii hao kwa kipindi tofauti kama miito ya wateja wao na kufanya biashara bila idhini ya wasanii husika.
Hakimu Mkazi Mwanadamizi wa Mahakama ya Ilala, Juma Hassan alitoa hukumu hiyo April 11 mwaka jana, baada ya kuendeshwa kwa kesi hiyo kwa kipindi cha miaka minne. Mbali na shilingi bilioni 2, Tigo waliamriwa kuwalipa wasanii hao shilingi milioni 25 zingine.





Tumeghaili hatuendi nje, tutaweka kambi mikoani – Yanga



 Uongozi wa klabu ya Yanga umesitisha mpango wa kuipeleka timu hiyo nchini Zambia kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa ngao ya hisani  dhidi ya Simba na maandalizi ya msimu mpya ujao.


Uongozi wa Yanga umesema badala ya kwenda Zambia sasa wanafikiria kuweka kambi kwenye mikoa kati ya Morogoro au Arusha ili kujifua kwa ajili ya maandalizi ya usimu ujao.
Timu itaingia kambini jumanne ijayo lakini sio nje ya nchi, mapendekezo yapo kati ya mikoa ya Arusha na Morogoro, mpaka kufika kesho au kesho kutwa tutajua tutaenda wapi,“amesema Kiongozi mmoja wa Yanga ambaye hakutaka jina lake liandikwe.
Kwa upande mwingine Kiongozi huyo amesema klabu ya Yanga bado ipo kwenye mchakato wa kumtafuta beki mbadala wa Vicent Bossou aliyetemana na klabu hiyo.
Sio kwa Bossou tuu pia Kocha Lwandamina bado hajaridhishwa na kiungo Justin Zulu na amepanga pia kumtafutia mbadala wake“,amesema Kiongozi huyo.
Wakati klabu ya Yanga ikijipanga kuweka kambi mikoani watani wao wa jadi Simba SC wana wiki moja sasa nchini Afrika Kusini walikoweka kambi wakijifua na mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa 2017/18.
Yanga na Simba zitavaana Agosti 23 mwaka huu kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa uwanja wa Taifa, jijini Dare se salaam kabla ya kufungua pazia la Ligi kuu Soka Tanzania bara dhidi ya Lipuli FC.

Alhamisi, 20 Julai 2017

Kizaazaa Dar mwanamke ‘atua’ uchi Airport










MWANAMKE mkazi wa Jiji la Dar es Salaam ambaye jina lake halikufahamika, amesababisha kizaazaa jijini, baada ya kushuka na ungo akiwa uchi wa mnyama.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na kushangaza watu kadhaa waliokuwa na taharuki, lilitokea juzi karibu na eneo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA).

Katika tukio hilo ambalo lilitokea majira ya mchana, mwanamke huyo alianguka katikati ya barabara katika eneo la  Ukonga Banana wilayani Ilala, akiwa kwenye ungo wake ambao alikuwa ameukalia bila kuvaa nguo.

Mwanamke huyo alikutwa amevaa sidiria yenye rangi nyeupe na kichwa alikuwa amefunga kilemba chenye rangi nyeupe.

Picha za mwanamke huyo zilianza kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na video akionekana amekaa katikati ya barabara.

Ungo aliokuwa ameukalia ulikuwa na unga huku akionekana akiongea na simu. Pia na kwenye masikio yake alionekana amevaa earphones.

Baada ya kugundua yupo katikati ya barabara, alinyanyuka na kwenda kuokota mizigo yake mingine ambayo ilianguka kandokando ya barabara hiyo, ukiwamo mkoba na viatu.

Makundi ya watu kadhaa walianza kumfuata huku mwanamke huyo akikimbilia kwenye kiwanja kilichopo TAA akiwa anajaribu kujificha viongo vyake visionekane kisha alichukua gauni lililokuwa kwenye begi na kuanza kulivaa.

Baada ya kuvaa, watu walianza kumzonga na kumzomea wakimuita mchawi na wengine wakaanza kumtembezea kichapo huku wakimuita mchawi.

“Mwanga, mchawi, muulize anatoka wapi. Kama ni mgonjwa mbona una zana… mchawi, mwanga,” walisikika wakimzonga.

Nipashe ilizungumza na mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini na kueleza kuwa mwanamke huyo anaishi karibu na Banana.

“Nimeelezwa anapoishi sio mbali, kumbe anajulikana na baadhi ya wanaomjua wamemshangaa kukutwa na tukio hilo lenye imani za kichawi, cha ajabu zaidi ameadhirika mchana,” alisema.

Taarifa ambazo hazikuthibitishwa zilidai kuwa mwanamke huyo alichukuliwa na Polisi kwa lengo la kumuokoa dhidi ya kichapo zaidi kutoka kwa wananchi waliokuwa na hasira.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, alipoulizwa jana kuhusiana na tukio hilo, alisema halijaripotiwa katika kituo chochote cha polisi.

Breaking News: Mama mzazi wa Zari afariki Dunia




Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Halima Hassan amefariki dunia asubuhi hii, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali.
Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinums, amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram, na haya ndiyo ameyaandika;
  
Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.

Jumatano, 19 Julai 2017

YANGA YAFANIKIWA KUMUONGEZA MKATABA KAMUSOKO




Baada ya mjadala mrefu, uongozi wa Yanga umefanikiwa kumuongeza mkopo kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.


Kamusoko ameongeza mkataba wa kuitumikia Yanga kwa miaka mingine miwili.

Mzimbabwe huyo kwa takribani wiki yote iliyopita alikuwa katika majadiliano na uongozi wa Yanga kuhusiana na mkataba wake mpya.

Leo kamati ya usajili imefanikiwa kumalizana naye na kasaini mkataba mpya mbele ya Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.

SIMBA FASTA, YAMALIZANA NA ERASTO NYONI KWA MIAKA MIWILI




Simba imemsajili beki wa kiraka, Erasto Nyoni kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyoni amejiunga na Simba akitokea Azam FC ikiwa ni siku chache baada ya kufanya vizuri katika michuano ya Cosafa.

Kitu kizuri kwa Nyoni ni uwezo wake wa kucheza namba zote nne za ulinzi.

Pia anaweza kucheza nafasi ya kiungo mkabaji kwa ufasaha hali inayomfanya kuwa na nafasi kubwa ya kucheza.

Nyoni alirejea nchini na kujiunga na Azam FC akitokea Vital'O ya Burundi.

BARTHEZ RASMI AACHANA NA YANGA NA KUTUA SINGIDA UNITED



Kipa Mustapha Ally Barthez amejiunga na Singida United.

Barthez amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Singida United.

Tundu Lissu agoma kutoka mahakamani



Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amegoma kutoka katika chumba cha mahakama ya wilaya ya Dodoma alipokuwa akifanya shughuli zake za uwakili akihofia kukamatwa na jeshi la polisi  kwa makosa ya uchochezi.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni rais wa chama cha mawakili Tanzania anasema amefikia uamuzi huo baada ya kubaini njama za polisi za kumkamata ambapo anadai awali askari wa jeshi hilo walifika nyumbani kwake Dar es Salaam na kumkosa na baada ya kuambiwa yuko Dodoma wamefika katika viwanja vya mahakama wakisubiri amalize shughuli zake na kisha wamkamate.

Aidha Mhe. Lissu amelitaka jeshi la polisi na baadhi ya viongozi wa serikali kuacha kukamata wanachama na wafuasi wa vyama vya upinzani ambao wanafanya mikutano ya ndani ya yenye lengo la kuimarisha vyama vyao kwani huku kufanya hivyo ni kukiuka demokrasia.

Mpaka ITV inaondoka mahakamani hapo majira ya saa kumi na nusu ambapo shughuli za mahakama zilikuwa zimemalizika Mhe. Lisuu alikuwa bado amesalia ndani ya chumba cha mahakama akiwa na baadhi ya wateja wake

Bibi wa miaka 86 ashtakiwa kwa wizi Marekani







 Doris Payne alikamatwa katika duka moja katika eneo la Chamblee mjini Georgia

Ajuza wa miaka 86 anayejulikana sana kwa wizi wa vito tangu miaka ya 50 ameshtakiwa kwa wizi.

Doris Payne alikamatwa katika duka moja katika eneo la Chamblee mjini Georgia kwa wizi wa vito vyenye thamani ya dola 86 kulingana na maafisa wa polisi.

Alipatikana amevalia kifaa cha kumfuatilia mtu mguuni katika shtaka jingine la wizi wa dukani.
Payne amehudumia vifungo kadhaa kwa uhalifu aliotekeleza.

Anadaiwa kuiba vito vyenye thamani ya dola milioni 2 na akaangaziwa katika makala ya 2013.

Mfanyikazi mmoja wa duka alisema kuwa aliiba vitu kadhaa kutoka kwa duka la dawa , vifaa vya
 kielektroniki na katika duka la mboga.

Wakili wake Drew Finding alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema: Hiki ni kisa cha kipekee ikilinganishwa na visa vyengine vilivyopita.

Tunazungumzia kile bibi wa miaka 86 anachotaka ili kuweza kuishi kila siku, ikiwemo chakula na matibabu.

Hivi karibuni alikiri kuiba mkufu kutika duka moja huko Atlanta.

Alihukumiwa kifungo cha nyumbani na kupigwa marufuku kuingia katika maduka ya jumla katika eneo hilo.

Niyonzima akwea pipa kuifuata Simba Sauzi



 KIUNGO mpya wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, aliyesajiliwa akitokea Yanga, kwa mara ya kwanza ataungana na nyota wenzake wa timu hiyo, Julai 29, mwaka huu katika kambi ya timu hiyo nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

Niyonzima ametua Simba baada ya kumalizana na Yanga ambapo amemaliza mkataba huku pia klabu yake hiyo ya zamani ikiweka bayana kuwa haitaendelea naye kwa msimu ujao baada ya kushindwana kwenye masuala ya maslahi.

Simba kwa sasa wamejichimbia Sauz ambako wanaendelea na kambi yao ya siku 20 wakijiandaa na msimu ujao ambapo wanatarajiwa kurejea Agosti 6, mwaka huu kwa ajili ya siku ya Simba Day ambayo itafanyika Agosti 8, mwaka huu.

Chanzo cha ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumatano kuwa, Niyonzima aliyetokea APR ya kwao Rwanda kabla ya kutua Yanga, atatua Sauz kuungana na wenzake siku hiyo baada ya siku zake za kimkataba na Yanga kumalizika.

“Kwa mara ya kwanza Niyonzima atavaa jezi za Simba Julai 29, mwaka huu ambapo ataungana na wenzake nchini Afrika Kusini ambapo kikosi kimepiga kambi ya siku 20 ya kujiandaa na michuano mbalimbali kwa msimu ujao, ambapo rasmi mkataba wake na Yanga utakuwa umefika ukingoni.

“Lakini mashabiki wengi watamuona siku ya Simba (Simba Day) Agosti 8, mwaka huu ambapo ndiyo atatambulishwa rasmi kwao sambamba na nyota wengine ambao tumewasajili hivi karibuni,” kilisema chanzo hicho.

Inaelezwa Haruna Niyonzima ameshasaini mkataba wa miaka miwili Simba kwa dau la dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 110 za Tanzania. Lakini Simba wanavizia mkataba wake Yanga uishe kabla ya kumtangaza kwa kuhofia adhabu ya kumsainisha mkataba akiwa ndani ya mkataba

chanzo gazeti la champion

Ukatili dhidi ya watoto waongezeka CAR-UNICEF




Watoto nchini CAR waliosambaratishwa na vita na kuhitaji msaada wa haraka. Picha: WFP/Alexis Masciarelli
Visa vya ukatili dhidi ya watoto, ikiwemo ubakaji, kutekwa nyara mauaji na kusajiliwa watoto katika vikundi vilivyojihami, vimeongezeka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), sanjari na kuzuka upya kwa mapigano,  limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, kama atavyotujuza John Kibego katika ripoti ifuatayo.
(Taarifa ya John Kibego)
Shirika hilo limesema huenda visa vya ukatili dhidi ya watoto katika miezi mitatu iliopita, vikawa vingi kuliko ilivyoripotiwa, kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama na kukatishwa kwa shughuli za kibinadamu katika meoneo mengi.
Aidha, taarifa za UNICEF zinaonyesha kuwa tangu mwezi Mei, vikundi vilivyojihami vimekuwa vikiwalenga watoto katika mashambulizi kwenye vijiji na miji.
Katika visa tofauti kule Bria, Mashariki mwa nchi, wasichana 14 wa umri kati ya miaka 9 na 16 walibakwa katika mapigano ya Mei na Juni, halikadhalika watoto watano wenye umri kati ya miaka miwili na 16 waliuauwa kinyama Bangassou, Kusini Mashariki mwa CAR mnamo Mei walipokuwa wakijaribu kukimbilia nchini DRC.
Wengine 17 walitekwa nyara akiwemo mmoja ambaye tayari ameripotiwa kuuwawa.

Taarifa mpya kuhusu Watoto Majeruhi wa ajali Arusha



 Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye anaratibu mchakato mzima wa matibabu ya Watoto watatu Nchini Marekani, waliojeruhiwa katika ajali ya Basi la Shule ya Lucky Vincent ya Arusha iliyoua wanafunzi 32, kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa huo amesema hali za watoto hao zimeimarika na kwamba Wanatarajiwa kurejea nchini Tarehe 18/8/2017 siku ya Ijumaa majira ya saa tatu Asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Kuhusu kama watoto hao mpaka sasa watakuwa wameelezwa chcochote kuhusu ajali iliyowakuta, Nyalandu amelijibu swali hilo

Clement Sanga ateua wajumbe wapya Yanga SC



 Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga ameteuwa wajumbe wapya 12 watakaounda kamati ya mashindano.


Katika wajumbe hao wapya waliyoteliwa, Magid Suleiman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti na Mustapha Urungo kuwa Makamu Mwenyekiti.