Jumapili, 4 Februari 2018

Mnyama ‘Simba SC’ hakamatiki, Maafande wa Ruvu Shooting watafunwa

Klabu ya Simba imeendeleza ubabe kwenye mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa kwa ushindi mnene wa goli 3-0 dhidi ya Maafande wa ‘Ruvu Shooting’.

Magoli ya Simba yamefungwa na Nahodha wa timu hiyo, John Bocco magoli mawili huku goli la tatu likifungwa na Mzamiru Yassin.
Kwa ushindi huo Simba inajidhatiti kileleni kwa alama 38 ikifuatiwa na klabu ya Azam FC alama 33, Mahasimu wao Yanga wakisalia nafasi ya tatu na alama 31.

Wastara amwaga chozi akiaga kwenda kutibiwa ‘Sijawahi kuchangiwa na Watanzania’

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wastara ameondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake ulioanza kumsumbua mwishoni mwa mwaka jana huku akiwashukuru watanazania na Vyombo vya Habari kwa kuwa pamoja naye kipindi alivyokuwa akihitaji msaada wa fedha.
Wastara
Wastara akiongea na waandishi wa Habari mapema leo Jumapili Februari 4, 2018 katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, amesema “nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia”. 
Na alipoulizwa kuhusu tuhuma za kutumia fedha za matibabu kwa starehe kama alivyowahi kuchangiwa kipindi cha nyuma na kwenda Dubai, Wastara amesema hajawahi kuchangiwa na Watanzania bali alisaidiwa Makamu wa Rais na hakutumia kwa matumizi mengine.
Kwanza niseme sijawahi kuchangiwa na Watanzania mimi kama mimi, mara ya kwanza nilipoumwa aliyenichangia asilimia kubwa alikuwa ni Makamu wa Rais, na uzuri ni kwamba mpaka nafika hospitalini nilikuwa nampigia simu. Kilichosababisha watu waseme baada ya kufika hospitali kama hivi ninavyokwambia wiki tatu linapotokea tatizo kama umefanyiwa Oparesheni au upasuaji wowote niliambiwa unauwezo wa kukaa au kuishi kwenye hoteli karibu na hospitali..Ndipo watu wa karibu yangu wa Oman wakawa wamenipa Visa nikaenda kukaa huko kwa muda.“ameongea Wastara.

Misri: Kaburi la miaka zaidi ya 4 400 lagunduliwa

Kaburi la miaka zaidi ya 4 400 limegunduliwa mjini Cairo , kaburi bila shaka liliandaliwa katika kipinidi cha  firauni,  cheo cha wafalme wa zamani wa Misri katika historia ya bara la Afrika.

Halid el-Anani , waziri  anaehusika na masuala ya kistoria nchini Misri alifahamisha katika mkutano ambao ulihudhuriwa  na mabalozi kutoka katika mataifa tofauti, alisema kuwa kaburi la miaka zaidi ya 4 400 limegunduliwa El-Cebane.

Dakika ya 75: #LaLiga Espanyol 1-0 Barcelona.

Image may contain: text

Hii hapa orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa upachikaji wa mabao katika #VPL msimu huu ikionesha Shiza Kichuya kuwa kinara wa kutoa pasi za mwisho (Assists)

No automatic alt text available.

#VPL @Johnbocco19 anaweka kimiani goli lake la pili katika mchezo wa leo na goli la tatu kwa Simba SC. 79' Ruvu Shooting 0-2 Simba.

Image may contain: text

#VPL Mzamiru Yassin anwaandikia Simba SC goli la pili katika dakika 66 kufuatia krosi safi ya Shiza Kichuya. 68' Ruvu Shooting 0-2 Simba.

Image may contain: text

Rais Magufuli ataka Viongozi wa Dini kujiepusha na migogoro

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo February 4, 2018 amehudhuria Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu wa Tano wa Dayosisi ya Dar es Salaam Askofu Jackson Sosthenes Jackson katika Kanisa kuu la Mtakatifu Albano Upanga.
Rais Magufuli amewataka viongozi na waumini wa madhehebu ya dini nchini kujiepusha na migogoro ambayo imekuwa ikiharibu sifa na heshima ya taasisi hizo muhimu katika jamii.
JPM amesema viongozi wa Serikali husikitishwa na uwepo wa migogoro katika madhehebu ya dini, na hupata mashaka kama kweli viongozi wa madhehebu husika wanazingatia matakwa ya Uchungaji.
Amempongeza Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dr. Jacob Chimeledya kwa kuumaliza mgogoro uliokuwa ukilikabili Kanisa hilo na hatimaye kufikia hatua ya kumweka wakfu Askofu Jackson Sosthenes Jackson kuwa Askofu wa Tano wa Dayosisi ya Dar es Salaam.
Rais Magufuli amemtaka Askofu Jackson Sosthenes  kuwa Askofu wa wote, kuvunja makundi yaliyokuwepo katika Dayosisi hiyo, kutolipiza kisasi na kusamehe yote yaliyopita na badala yake ajenge Dayosisi imara na aongoze kwa haki na upendo kwa wote.

Pia JPM amewahakikishia viongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na kanisa hilo na madhehebu mengine ya dini katika shughuli zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii kama vile hospitali, na shule.
Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson Mwansasu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu  Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.

Siku ya kimataifa ya Saratani duniani 2018

Mama mkimbizi katika kambi ya Dadaab, Kenya akiwa na mtoto wake ambaye anaugua ugonjwa wa saratani. UM/Evan Schneider (maktaba)
Siku hii ya saratani inaadhimishwa kila mwaka Februari 4 na  ya mwaka huu  inakuja wakati  ripoti zinasema imeshakatili maisha ya watu milioni 14 duniani.
Shirika la afya duniani-WHO linasisitiza kuwa karibu kila familia duniani inaguswa na saratani kwa njia moja au nyingine lakini wakati huu kuna maendeleo fulani  ambayo yamepatikana kuhusu tiba ya saratani.
Licha ya hivyo WHO inasema mbali ya  kupatikana maendeleo katika juhudi za kuzuia, kutibu na kutoa tiba shufaa kwa wagonjwa  wa saratani, lakini maendeleo hayo hayapatikani kote duniani.
Katika tarifa yake kwa ajili ya siku hii shirika hilo linasema matibabu katika nchi nyingi baado ni ghali mno au hayapatikani kamwe na pia huduma za tiba shufaa hazipo.
Kwa mujibu wa takwimu za WHO, saratani ndio iliongoza dunaini kama chanzo cha magonjwa  na vifo mwaka 2012 na kulikuwa na visa vipya takriban milioni 14. Aidha mwaka 2015 saratani  ilishika nafasi ya pili kwa kusababisha  vifo 14 milioni huku asilimia 70 ya vifo vyote vya saratani hutokea katika mataifa  yenye vipato vya nchini na wastani.
Mbali na tiba wataalamu wanasema kuwa theluthi moja ya vifo vya saratani  hutokea kwa sababu 5 muhimu za kitabia pamoja na aina fulani ya vyakula zikiwemo mwili mnene kupita kiasi,  ulaji mdogo wa matunda na mboga za majani, kutofanya mazoezi, utumiaji wa tumbaku na pombe.
WHO inaamini kuwa mwaka 2018 utakuwa mwaka muhimu ikifafanua kuwa mataifa wanachama yatakuwa yakitekeleza miongozo ya azimio la kikao cha  afya duniani ,pamoja na ripoti ya maendeleo ya kupatikana kwa ratiba ya utekelezaji wa azma za mataifa  katika mkutano wa ngazi za juu wa tatu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoyakuambukiza , ambao utakafanyika katika nusu ya pili ya mwaka 2018.

Ratiba rasmi ya mazishi ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

Jumapili tarehe 4/2/2018
- Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street, Dar es salaam.

-Saa 11:00 Jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)

******************************
Jumatatu tarehe 5/2/2018
- Saa 1:00 Asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
- Saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
- Saa  4:00  Asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu
- Saa 6:00 Mchana mwili kuwasili Karimjee hall kwa shughuli ya kuagwa
- Saa 6:00 Mchana  9:00 Alasiri kuaga mwili wa marehemu
- Saa 9:00 Alasiri mpaka 9:30 Alasiri msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni
- Saa 9:30  Alasiri mpaka 11:30 Jioni maziko
- Saa 11:30 Jioni 12:30 Jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa chakula cha jioni kwa waombolezaji wote
1:30 mpaka  2:45  Usiku chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 Usiku-Hitimisho la shughuli ya Mzee wetu kwa waombolezaji wote.

Tunawashukuru sana waombolezaji wote kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu. Mungu awazidishie.

Bwana ametoa, na bwana ametwaa.
Jina lake na lihimidiwe - AMINA

Imetolewa na:
Omary A. Kimbau

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi

#VPL Dakika 10 zimeshakatika katika dimba la Kambarage, Shinyanga na mpaka sasa 'si wenyeji Stand United, si wageni Mtibwa Sugar'. 10' Stand United 0-0 Mtibwa Sugar.

Image may contain: text

Padri wa Kanisa Katoliki atekwa nyara


Leo February 4, 2018 Polisi wanadaiwa kumteka nyara Padri Sebastian wa kanisa Katoliki baada ya ibada kumalizika ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa za mashuhuda waliokuwa nje ya Kanisa katika Mji mkuu wa Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Hayo yanatokea wakati mivutano kati ya kanisa Katoliki na serikali ya DRC ikizidi kushika kasi kufuatia hatua ya Rais Joseph Kabila kukataa kuondoka madarakani baada ya muda wake kwa mujibu wa katiba kumalizika.
Shuhuda mmoja katika kijiji cha N`sele mashariki mwa mji wa Kinshasa amelieleza shirika la habari la AFP kuwa polisi walimkamata Padri Sebastian Yebo baada ya Ibada ya asubuhi na kumpakiza kwenye gari aina Jeep na kuondoka naye.
Hata hivyo Polisi walikataa kuzungumzia tukio hilo walipoulizwa na shirika la habari la AFP. Tukio hilo linakuja ikiwa ni baada ya operesheni iliyofanywa na serikali dhidi ya waratibu wa maandamano ya waumini wa kanisa Katoliki kupinga rais Kabila kuendelea kubakia madarakani.

TRA yafungia hoteli tatu Mtwara



Mamlaka ya Mapato mkoani Mtwara (TRA) imezifungia hotel tatu mkoani humo pamoja na kituo cha kuuza mafuta kwa kushindwa kulipa kodi ya malimbukizo ya madeni.
Hotel zilizofungiwa ni Naff Beach, Naf blue, BNN pamoja na kituo cha Mnarani Petrol Station ambao kwa pamoja wanadaiwa zaidi ya Shilingi 1 bilioni ambazo ni malimbukizo ya madeni ya nyuma kwa kipindi cha miaka mitatu.
Afisa Mwandamizi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Mtwara, Flavian Byabato amesema zoezi hilo ni endelevu kwa mkoa mzima.