Jumanne, 5 Juni 2018

TUHUMA ZA KUBAKA WANAFUNZI WALIMU ,WAFANYAKAZI KUCHUNGUZWA







Image may contain: 1 person, standing and text
 Walimu pamoja na wafanyakazi wengine wa kiume katika Shule ya Sekondari ya wasichana ya Moi jijini Nairobi wametakiwa kufanyiwa uchunguzi wa DNA kwa ajili ya uchunguzi wa tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo Ijumaa usiku.
Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, walinzi na jamaa wa kiume wa walimu wanaoishi ndani ya shule hiyo au wale wanaoaminika kuwa walikuwa ndani ya shule hiyo mapema Jumamosi asubuhi kuchukuliwa vipimo hivyo.
Uchunguzi huo wa DNA ni muhimu katika kubaini kesi za unyanyasaji wa kingono na hutumika kumgundua mshukiwa dhidi ya maji maji yanayopatikana katika mwili wa mwathiriwa na hivyo kuweza kuwa na ushahidi mzito katika kesi.
Polisi wanajaribu kuchunguza matukio yaliojiri usiku huo na siku ya pili kujua ukweli upo wapi katika tuhuma hizo za kubakwa kwa wanafunzi hao wa kike wa Moi ambazo zimeamsha hasira kubwa nchini.
Maafisa hao pia wanachunguza kuhusu tuhuma kwamba uongozi katika shule hiyo uliwaambia wanafunzi walitendewa vitendo hivyo kujisafisha na kutosema chochote kuhusu kinachotuhumiwa kutokea.







Image may contain: 4 people, people smiling, outdoor

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni