Ijumaa, 8 Juni 2018

"Siwezi kusubiri mpaka nife" - Haji Manara



Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Mabingwa wa Ligi Kuu (VPL) Simba SC, Haji Manara amefunguka na kudai anajifahamu yeye binafsi kuwa ndiye msemaji pekee ndani ya wekundu wa Msimbazi na hawezi kusubiri mpaka afe ndio aweze kusifiwa kwa afanyacho.
Manara amesema maneno hayo yenye ukakasi kupitia ukurasa wake wa kijamii huku baadhi ya watu wakimuunga mkono juu ya maneno yake hayo lakini wengine wakionekana kutopendezewa nayo kwa namna moja ama nyingine.
"Sisubiri nife ili mnisifu, najijua 'my self' kuwa mimi ni msemaji wa klabu wa muda wote ndani ya nchi hii ya Tanzania kwa vigezo vyovyote vile hakuna hata wa kukaribia robo. Ukibisha lazima wewe ni mwanga", ameandika Manara.
Kutokana na kauli hiyo ya Manara, baadhi ya wafuasi wake katika mtandao wake wamemuomba kiongozi huyo kumshauri swahiba wake Jerry Muro aweze kurudi katika nafasi yake ya usemaji wa klabu ya Yanga SC ili wapate kujibizana vizuri kama walivyokuwa wanavyofanya hapo awali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni