Serikali
ya Tanzania imelitaka Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la
Kilutheli Tanzania (KKKT) Tanzania kufuta waraka lililoutoa wakati wa
mfungo wa kwaresma kwa madai kuwa Baraza hilo halina mamlaka kisheria ya
kutoa waraka huo.
Leo
Juni 6, 2018 imesambazwa barua inayoonyesha imeandikwa na Wizara ya
Mambo ya Ndani kwenda kwa mwenyekiti /askofu mkuu wa KKKT iliyoandikwa
Mei 30, 2018 ikitoa maelekezo ya kufutwa waraka huo ndani ya siku 10
tangu ilipoandikwa barua hiyo.
Ikiwa na kichwa cha habari ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa KKKT’ barua hiyo inaeleza baraza hilo halitambuliki kisheria katika ofisi ya msajili.
Aidha, barua hiyo inaeleza kuwa Katiba inayotumiwa na Kanisa hilo ni ya mwaka 1960 ambayo ilipitishwa na msajili mwaka 1963. Hivyo Serikali inalitaka Kanisa hilo kuomba kibali cha kufanya marekebisho ya katiba hiyo.
==>Bado tunaendelea kufuatilia uhalisia wa barua hiyo ambayo iko hapo chini na tutaendelea kukujuza.

CHANZO MPEKUZI BLOG
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni