Jumatano, 6 Juni 2018

Sababu za Chura kufungishwa Ndoa India

Dunia ina vituko sana leo June 6, 2018  nakusogezea stori kutoka mji wa Lagaan nchini India ambapo wakazi wa eneo hilo huwafungisha ndoa CHURA kama ishara ya kumuomba Mungu wao wa mvua awaletee Baraka za mvua katika eneo hilo.
Unaambiwa kuwa katika mji wa Lagaan mvua ndio kila kitu na wakazi wa eneo hilo wako tayari kufanya lolote lile ili tu kumfurahisha Mungu wao mvua.
Aidha inaelezwa kuwa katika zoezi la kuwafungisha ndoa CHURA wakazi wa eneo hilo hufanya sherehe kubwa sana ambapo chura mwanaume na mwanamke huandaliwa na kupambwa vizuri kabla ya kufungishwa ndoa na kuhani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni