Alhamisi, 7 Juni 2018

Ridhwan Kikwete “Tangulia rafiki yangu ‘Mwana wa ukae”

Msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Chanzo cha kifo chake kimelelezwa na Producer wake Steve kuwa “Sam alianza kuzidiwa toka J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema ukimwi lakini sio ukimwi wa kawaida bali wa kulogwa”

Mwili wa marehemu umepelekwa katika hospitali ya Mwananyamala kuhifadhiwa.

 
Leo June 7, 2018 Mbunge wa Chalinze Ridhwan Kikwete amezipata taarifa za kifo cha hitmaker wa ‘Hata kwetu wapo’ Sam wa Ukweli na ameamua kuandika katika ukurasa wake wa Twitter.
Ridhwan ameandika “Innallillah Wainnaillah Rajuun, Nadhani sihitaji kusema mengi ila kumshukuru Mungu Mwenyezi kwa mapenzi yake kwetu Binadamu na hasa kwako rafiki yangu Sam “Mwana Wa Ukae, Mzukulu wa Mwali Bonele Wa Kiwangwa”.Tangulia Rafiki Yangu, Pumzika kwa Amani Sam Wa Ukweli.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni