Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Rais wake, Mwigulu Nchemba, umempanga kumtumia tiketi mshambuliaji wa kimataifa kutoka Benin, Marcellin Koukpo ambaye alitajwa kutua Yanga.
Singida wameingia kwenye rada na mshambuliaji huyo ambaye ilielezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na mabingwa mara 27 wa ligi kuu bara, Yanga.
Taarifa zinasema kuwa Singida wamepanga kumtumia tiketi ya ndege ili kumuwezesha Koukpo aweze kutua hapa nchini tayari kumalizana naye mapema ili aanze kuitumikia klabu hiyo.
Wakati Singida wakitaka kuiharibia Yanga mipango hiyo ya usajili wa mchezaji huyo, uongozi wake kupitia Boniface Mkwasa umekuwa ukilalamika kuhusiana na kuchukuliwa wachezaji wake ambao wamekuwa wakiwataja ili waweze kuwasajili.
Kitendo hicho kilimuibua Mkwasa na kueleza kuwa hawatothubutu kuweka wazi nani na nani wanataka kusajili na badala yake watafanya kimyakimya ili kuzinyima nafasi timu ambazo zimekuwa zikiwaibia wachezaji hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni